Machapisho

HISTORIA YA MWANAMALUNDI

HEBU LEO MJUE VIZURI HUYU MTU WA MIUJIZA AITWAE NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAJERUMANI. Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwanza. ...

SHAIRI LA SIBANDUKI

SIBANDUKI Kama kidole na Pete, Au ulimi na mate, Milele takuwa wote, SIBANDUKI . Mapigo yenda ta ta ta, Mie kwako ni zezeta Wala siwezi kujuta, SIBANDUKI. Mtasema msemavyo, Kuchongea mjuavyo, Nitabaki hivyo hivyo, SIBANDUKI . Tumependana wenyewe, Tunapeana wenyewe, Tunafurahi wenyewe, SIBANDUKI . Waongee Siku kucha, Penzilo halitochacha, Daima sitakuacha, SIBANDUKI . Waseme maneno yote, Ya duniani kote, Hadi wakauke mate, SIBANDUKI . Kiangazi na masika, Siku mwezi na miaka, Kwa kimbunga na ghalika SIBANDUKI . Hata nichomwe mikuki, Au risasi lukuki, Kwako mwandani sing'oki, SIBANDUKI . Mahakama za kitaifa, Au za kimataifa, Waninyonge hadi kufa, SIBANDUKI .

Uhusiano wa Sintaksia na Matawi mengine ya Isimu

Dhana ya sintaksia imejadiliwa na wanazuoni mbalimbali ;             Massamba na wenzake (1999:34) anasema “sintaksia ni utanzu wa sarufi unaojihusisha na uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa vipasho vyake”. Wanaendelea kusema, utanzu huu huchunguza sheria   au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ili yalete maana inayokubalika na kueleweka katika lugha husika.            Habwe na Karanja (2004) wanasema “sintaksia ni utanzu wa isimu unaoshughulikia muundo wa sentensi na elementi nyingine zinazounda sentensi kama vile kategoria za maneno, vikundi na vishazi”         TUKI (2004)anasema “sintaksia ni tawi la isimu linaloshughulikia uchanganuzi wa taratibu na kanuni za mahusiano baina ya maneno katika tungo” kwa ufupi sintaksia ni tawi la isimu ambalo linachunguza muundo wa tungo pamoja na uhusiano wa v...

Dhana ya Nadharia

Dhana ya nadharia imejadiliwa na wanazuoni mbalimbali ambao wamekuja na mitazomo tofauti tofauti kama ifuatavyo;            Kwa mujibu wa Wamitila, (2003:22) “nadharia ni mawazo, dhana au maelezo yanayotolewa kuelezea hali fulani : chanzo chake, muundo wake, utenda kazi wake na mwingiliano wake wa ndani na nje”           TUKI (2004:300) wanasema “nadharia ni mawazo, maelezo au mwongozo uliopangwa ili kusaidia kueleza, kutatua au kutekeleza jambo fulani” Fasili hii ya TUKI inafanana kwa kiasi fulani na fasili ya Mdee (2011) anayefasili nadharia kuwa ni mpango wa maneno uliotungwa ili kuelekeza jinsi ya kufanya au kutekeleza   jambo fulani. http://kapeleh.blogspot.com/2014/05/nadharia-za-maana.html Kwa msingi huo nadharia hubeba mawazo ,dhana au maelezo yatolewayo kwa nia au lengo la kueleza hali fulani, chanzo,muundo, utendaji na mwingiliano wa ndani na nje. Kuna nadharia ...