Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2017

HISTORIA YA MWANAMALUNDI

HEBU LEO MJUE VIZURI HUYU MTU WA MIUJIZA AITWAE NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAJERUMANI. Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwanza. ...

SHAIRI LA SIBANDUKI

SIBANDUKI Kama kidole na Pete, Au ulimi na mate, Milele takuwa wote, SIBANDUKI . Mapigo yenda ta ta ta, Mie kwako ni zezeta Wala siwezi kujuta, SIBANDUKI. Mtasema msemavyo, Kuchongea mjuavyo, Nitabaki hivyo hivyo, SIBANDUKI . Tumependana wenyewe, Tunapeana wenyewe, Tunafurahi wenyewe, SIBANDUKI . Waongee Siku kucha, Penzilo halitochacha, Daima sitakuacha, SIBANDUKI . Waseme maneno yote, Ya duniani kote, Hadi wakauke mate, SIBANDUKI . Kiangazi na masika, Siku mwezi na miaka, Kwa kimbunga na ghalika SIBANDUKI . Hata nichomwe mikuki, Au risasi lukuki, Kwako mwandani sing'oki, SIBANDUKI . Mahakama za kitaifa, Au za kimataifa, Waninyonge hadi kufa, SIBANDUKI .